NEEC YASHIRIKI MAONESHO KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI ARUSHA
Imewekwa: 05 Mar, 2025
NEEC YASHIRIKI MAONESHO KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI ARUSHA

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linashiriki katika maonesho ya wiki ya wanawake kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika Mkoani Arusha tarehe 8 mwezi wa 3 mwaka huu.

Baraza linashiriki katika maonesho hayo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu fursa zinazopatikana nchini hasa katika miradi ya kimkakati. Vile vile wananchi wa Mkoa wa Arusha na Mikoa jirani watapata fursa ya kuifahamu mifuko ya Uwezeshaji inayopatikana nchini ambayo inasimamiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Kilele cha maonesho hayo kitafanyika siku ya wanawake duniani ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi. Mgeni rasmi katika kilele hicho anatarajiwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan. Kaulimbiu ya mwaka huu ni 'WANAWAKE NA WASICHANA 2025, TUIMARISHE HAKI USAWA NA UWEZESHAJI'

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo